UJUMBE MAALUMU KWAKO MARCH 19, 2021.
HATA KATIKA HILI BADO WEWE NI MUNGU WETU
Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA.
FUATANA NASI FACEBOOK:👉🏼 https://bit.ly/FacebookHUSONEMU
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Moyoni mwangu nimeona nikutumie ujumbe huu katika kipindi hiki kigumu.
Unaweza kuwa na maswali mengi mnoo kwanini hili limetokea nchini Tanzania?
Kwanini Mungu aruhusu kitu kama hiki wakati mataifa yoote wanatutazama kwa sura ya ajabu kuwa Mungu wa Tanzania ni Mungu wa kuokoa?
Unaweza kusikia kelele za shetani na mazomeo ya wajumbe wake wasemao yuko wapi Mungu wao?
Usione ajabu neno hilo tokea zamani shetani hua analitumia neno hilo. Angalia mistari hii. “ Kwa nini mataifa kusema, Yuko wapi Mungu wao?”(Zaburi 115:2)
Angalia mistari hii mingine”Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?”(Zaburi 42:10)
Ukiona mtu yoyote anakejeli kitendo cha watu kumuomba Mungu fahamu nyuma yake kuna mtesi yaani shetani... sijakosea nyuma yake kuna shetani...
Mtesi huitumia lugha hiyo tokea siku nyingi pale anapowashambulia watu wamuombao na kumtegemea Mungu. Ili awakatishe tamaa hutumia neno hilo yuko wapi Mungu waombona hajawasaidia nk....
Mungu anataka wewe utafute msaada kwake, Mungu anataka taifa litafute msaada kwake.
Msikie asemavyo “ BWANA akamtokea Sulemani usiku, akamwambia, Nimesikia uliyoyaomba, na mahali hapa nimejichagulia kuwa nyumba ya dhabihu. Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni;ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”(2Nya 7:12-14)
Ikitokea shida iwe kwako au kwa taifa lako Mungu anataka tumtafute yeye tumuombe yeye ili atatue tatizo hilo.
Ukiona mtu anajaribu kukutoa kwenye wazo la kumtafuta Mungu kwenye shida yako au shida ya taifa lako nakushauri muogope mtu huyo...nyuma yake kuna mtesi yaani shetani.
Unaweza kuwa na swali mbona sasa tulimtafuta Mungu katika shida yetu? Na mimi nataka nikuulize swali tulipomtafuta hakuonekana? Jibu ni rahisi tu alionekana.. alilivusha taifa hili katika gumu hilo na hata hii awamu ya pili pia baada ya kumtafuta Mungu bado Mungu ameonekana.
Ukiangalia hali ilivyo utaona wazi shida ile iliyolikabili taifa letu kwa awamu ya pili ya maambukizi na vifo imeshuka mnoo... Kwa maana nzuri Mungu ameonekana.
Swali kwanini Mungu huyu tunayemtafuta aruhusu mleta hoja ya kumtafuta Mungu afe katika kipindi hiki? Naamini unaswali hilo moyoni mwako na maswali mengine mengi tuuu yamkini yamekujaa moyoni.
Unajua Kuna maswali kabla hauja muuliza Mungu unatakiwa umuombe msamaha kwanza, kwasababu unaweza kumuuliza au kumueleza jambo ukajikuta unamuudhi...
Ntakupa mifano uone hili ninalokufundisha Angalia mistari hii. “Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini.Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.”(Mwanzo 18:30-32).
Ibrahimu alijua wazi kuwa kuna maswali ambayo ukimuuliza Mungu anaweza kukasirika, kabla hajauliza hilo swali alinza kushughulika kwanza na kutengeneza mazingira ya kumfanya Mungu asimkasirikie anapolisikiliza swali la Ibrahimu.....
Ibrahimu alijua kuwa kuna maswali au maneno au mawazo tunayoweza kuyawaza au kuyasema mbele za Mungu ndani yake huzalisha hasira kwa Mungu.
Na kwambia ukweli kuna mazungumzo kati yako na Mungu yanaweza kuzalisha hasira kwa Mungu dhidi yako... Angali mfano huu “BWANA akamwambia, Ni nani aliyekifanya kinywa cha mwanadamu? Au ni nani afanyaye mtu kuwa bubu au kiziwi, au mwenye kuona, au kuwa kipofu? Si mimi, BWANA? Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena. Akasema, Ee Bwana, nakuomba, tuma kwa mkono wake huyo utakayemtuma. Hasira ya BWANA ikawaka juu ya Musa, akasema, Je! Hayuko Haruni, ndugu yako, Mlawi? Najua ya kuwa yeye aweza kusema vizuri. Pamoja na hayo, tazama, anakuja kukulaki; naye atakapokuona, atafurahi moyoni mwake. “( Mwanzo 4:11-14)
Katika maneno hayo tunajifunza wazi kuwa tunahitaji kuwa makini mnoo katika maswali yetu mengi tunayomuuliza Mungu.... unajua ni kwanini?
Kuna maswali kabla hatujauliza yanaonekana ni mazuri mnoo... lakini ukitulia na kuyaangalia hayo maswali ndani yake huwa yanabeba picha ya kutokumuamini Mungu... yanakua ni maswali yanayoonyesha kuwa Imani ya mtu aliyokua nayo kwa Mungu sasa haipo tena.
Ntakupa mfano huu uone. Yohana mbatizaji yeye ndiye alitumwa ili amshuhudie Bwana Yesu Kristo kwa Wana wa Israeli.
Angalia mistari hii. “Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu. “(Yohana 1:29-34)
Yohana huyu siku moja alijikuta akipitia gumu mnoo ambalo lilimletea swali moyoni mwake...bahati mbaya swali lile lililokua ndani yake yeye hakujua kuwa litamtengenezea picha ya ajabu machoni pa Mungu
Angalia mistari hii uone hiki ninachokuambia. ‘Ndipo Yohana alipowaita wawili katika wanafunzi wake, akawatuma kwa Yesu akiuliza, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? Nao walipofika kwake, walisema, Yohana Mbatizaji ametutuma kwako, akisema, Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine?Na saa ile ile aliwaponya wengi magonjwa yao, na misiba, na pepo wabaya; na vipofu wengi aliwakirimia kuona. Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema.Naye heri mtu ye yote asiyechukizwa nami.”(Luka 7:19-23)
Ukiliangalia swali la Yohana utaliona ni swali zuri tu, ukitulia na kulitazama swali hilo utaliona lilikua ni swali ambalo lilijaa mashaka au kutokuamini. Na ndani ya swali hilo utaona kuna kuchukia ndani yake. Bwana Yesu Kristo alipolisikia swali lile alijua wazi kuwa Yohana alipoingia kwenye taabu yake amepata shaka na chuki furani hivi moyoni...
Unajua hata kwetu kama taifa, tunaweza kuwa na maswali ya picha hii hii ya kuonyesha shaka kwa Mungu wetu na hata kuwa na chuki kabisa...
Ngoja nikuulize swali katika hili lililotokea mshuhudiaji wetu aliyetushuhudia kuwa tukamuombe Mungu na sisi tukaamini tukaomba na Mungu kweli akajibu kaondoka katika kipindi hiki...je! Imani yako bado ipo kwa Mungu au imeingia shaka na chuki kwa Mungu?
Ukitaka kujua Upoje angalia maswali yako unayojiuliza weee... ukigundua ni maswali yaliyobeba mashaka kwa Mungu nakushauri tubu....
Mungu kuliruhusu hili litokee fahamu halimuondolei uhalali wa kuwa Mungu katika Taifa hili... Mungu kuliruhusu hili litokee halimuondolei uhalali wa kuwa Mungu aponyae Taifa hili..... Mungu kuliruhusu ili litokee halina maana sisi tu wakosa mnoooo....
Mungu ana akili za juu mnoo wapendwa, njia zake na mawazo yake yapo juu mnoo...unaweza kuwa na maswali ya kitoto kwa nini asingeliruhusu hili miaka ijayo ili jina lake litukuzwee? Ehehee…
Sikia jina lake limetukuzwa kabla ya misingi ya ulimwengu kuumbwa. Na hata sasa linazidi kutukuzwa tuuu... na hata baada ya hili jina la Bwana Yesu Kristo litazidi kutukuzwa tuuu.
Shetani asikudanganye kuwa Eti kwasababu ya hili Mungu kaahibika...eheheeee hajawahi haibika na hata aibika..ILA MTESI ATAAIBIKA TU....
NI KIPINDI CHA IMANI YETU KWA MUNGU KAMA TAIFA KUJARIBIWA
Sikiliza Imani ya taifa letu kwa Mungu sasa ipo kwenye mizani... ADUI ANAPOZOMEA FAHAMU NIA YAKE NI KUIFANYA MIZANI HIYO AITAWALE YEYE..
Sikiliza mwambie shetani kuwa HATA KWA HILI BADO MUNGU NI MUNGU WETU WA TANZANIA... NA TANZANIA NI YA MUNGU..
Kuna kipindi ulimwengu na nchi inaweza kupelekwa kujaribiwa.. Biblia inasema hivi. “ Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”(Ufu 3:10-11)
Taifa letu kwa sasa linapitia jaribu hili...tunachotakiwa tukifanye kama taifa ni kukishika kile tulichonacho yaani Bwana Yesu Kristo...
Jaribu lolote linaporuhusiwa likupate fahamu linatafuta kukuondolea IMANI YAKO KWA MUNGU.
Sikiliza kama Mtanzania usikubali kuondolewa hicho ulichokishika yaani IMANI YAKO KWA BWANA YESU KRISTO KAMA MSAADA WETU NK.
Ondoa hofu na shaka na wasiwasi...zidi kumpenda Mungu ondoa chuki kwake na usiache kuliombea Taifa lako...sikiliza nikwambie KUNA UTUKUFU MKUBWA TANZANIA.. ADUI ANATAFUTA KUINDOA TAJI TULIYOPEWA NA MUNGU KATIKA TAIFA HILI....
Adui anaporuhusiwa ayafanye hayo fahamu TUKIKAZA IMANI ZETU KWA MUNGU KUNA UTUKUFU MKUBWA ZAIDI MNOO KWA TAIFA LETU UNAKUJA.
Usikubali Mtanzania kuondoa imani yako kwa Mungu, endelea kumuombea Raisi ajaye na VIongozi wetu WAZIDI MNOO KUTUSHUHUDIA KUHUSU MUNGU KUTUSAIDIA.
Nimalizie kwa kusema HATA KWA HILI BADO MUNGU NI MUNGU WETU,Mungu akubariki sana inuka futa machozi... mtazame Mungu AMEN.
Wako
Mwl Steven & Beth Mwakatwila.