Wednesday, February 13, 2019

15.MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI

1⃣5⃣ MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI

Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA

FUATANA NASI:- APP, FACEBOOK, INSTAGRAM, ONLINE RADIO 📻, WHATSAPP, WEBSITE & YOUTUBE, Kwa links zilizoko kwenye HII LINK hapa:

KUPATA APP YETU “HUSONEMU (MWAKATWILA) APP” BONYEZA LINK HII HAPA:

🗓 13 Februari, 2019

KIPINDI CHA KUMI NA TANO (15).

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana naamini unaendelea vizuri. Naomba unisamehe kwa kukucheleweshea kukuletea somo hili.

Kwakweli nimekua na ratiba ngumu kidogo. Sasa leo nimeupata huu muda nimeona niutumie kukuandikia na kukutumia sehemu nyingine ya somo hili nililokuahidi kukuletea.

Katika somo lililopita nilikuonyesha kuhusu chanzo kingine kinachoweza kuwa kinapelekea mtu awe na tabia ya uzinzi nacho ni roho au pepo la uzinzi.
Sikiliza si kila uzinzi afanyao mtu chanzo chake ni pepo au ni mwili na tamaa yake ukiwemo huu uzinzi.

Laki hivyo vyanzo viwili kimoja wapo kinaweza kuwa ndiyo kinachozalisha au kumsukuma mtu kwenye tabia ya uzinzi.

Mapepo yanaweza kabisa kumtengenezea mtu tabia mbalimbali na mtu huyo akajikuta akizifanya hizo tabia bila yeye kuridhia. Ngoja nikuonyeshe mifano mingine naamini utanielewa vizuri sana.

Angalia mistari hii. ”Naye Yesu akiona ya kuwa mkutano unakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu, wala usimwingie tena. Akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka; naye akawa kama amekufa; hata wengi wakasema, Amekufa. Lakini Yesu akamshika mkono akamwinua naye akasimama”(Marko 9:25-27)”.

Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa pepo anapomuingia mtu anamfanya huyo mtu awe na tabia YA HUYO PEPO. Pepo bubu alipomuingia huyo mtu huyo mtu akawa bubu kabisa.

Angalia kitu hiki alipotolewa pepo huyo bubu huyo mtu akaanza kusema. Aisee, kumbe basi kuna watu leo hii wanatabia fulani ambazo zinaonekana kabisa katika mwili na tukafikiria kuwa ni huyo mtu alivyo kumbe mwenzetu kaingiwa na pepo la namna hiyo na ndilo linalomfanya huyo mtu awe hivyo.

Pepo la udhaifu likimwingia mtu fahamu huyo mtu atakua na udhaifu huo huo.

Angalia mistari hii “ Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa.Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako.Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu.Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu, akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato.Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye.”(Luka13:11-17)

Angalia pepo huyo waudhaifu alipoondolewa ndani ya huyo mtu maandiko yanatuambia udhaifu huo ulimwacha muda huo huo.

Ninachotaka nikuonyeshe ni namna roho mbaya au mapepo au shetani akimuingia mtu, mtu huyo hujikuta akifanya kile kilichobebwa na huyo pepo. Kama pepo limebeba tabia fulani ugonjwa fulani basi huyo mtu hujikuta anakua na ugonjwa huo huo mpaka siku pepo hilo limetolewa ndani ya huyo mtu.

Pia pepo la uzinzi linapomuingia mtu fahamu huyo mtu atakua hivyohivyo kama hilo pepo lilivyo. Mtu wa namna hiyo nakuambia ukweli atazini tuu hata na wanyama au namwanamke mwenzie au na wanaume watatu hata wanne kwa pamoja na hata mumshauri vipi hawezi kuwasikia.

Nakuambia atazini  kwa mikono yake ata fanya vitu ambavyo hata mtu akikusimulia huwezi kuamini. Ngoja nikupe mfano huu. Siku moja nilifuatwa na mama mmoja, akaniambia mjukuu wake anashida, unajua huyo mjukuu alikua bado ananyonya alikua wa kike. Yaani ni mdogo amebebwa mgongoni na bibi yake.

Nikamuuliza anashida gani yule mama alishindwa kuniambia, nikamuita mke wangu akaja, akamsimulia na mke wangu akaja kuniambia kuwa mtoto huyo anatabia ya kujisaga kwa kutumia mikono yake.

Yaani nilishangaa sana. Mtoto anayenyonya anafanya hivyo? Haraka nikajua tu hilo ni pepo la uzinzi limemwingia huyo mtoto. Unajua nikamchukua huyo mtoto yaani huwezi hata kumuuliza kitu kwasababu ni mdogo anajua kusema mama baba bibi na maneno machache sana.

Tulipoanza  kuomba toba tu, nilishangaa kuona huyo mtoto akianza kurembua macho na kweli alianza kujisanga sehemu zake za siri na akilifanya hilo tendo akitaka kujitoa nguo na nepi zake ili afanye vizuri yaani ilisikitisha sana.

Tukalikemea hilo pepo na kuliamuru limuachie huyo mtoto lilipomtoka tu huyo mtoto akawa vizuri na nilimuona akiwa kafunguliwa akimlilia bibi yake na alikua na amani na furaha fulani hivi.

Nilifikiria hivi ni watoto wangapi leo hii wanapepo la uzinzi na wazazi wao hawajui? Bibi huyu alipogundua hakuona aibu aliamua kumsaidia bibi yake akamleta kwangu  kama mtumishi wa Bwana Yesu Kristo.

Fikiria mtoto wa namna anakua binti? Unafikiri wanaume watapona hapo hasa wanaume ambao wanauendekeza mwili kweli? Naamini mtoto wa namna hiyo anaweza kuanza uzinzi akiwa mtoto mdogo mno na akakutana na mtu hata mzima tu akamvuta kipepopepo na akazini naye na huto mtu mzima akashikwa na kupigwa miaka mingi jela.

Nani atamuelewa huyo mtu mzima akisema jamani mwenzenu hata mimi nashangaa nimezini na katoto haka sijui nini kimenikuta, kumbe huyo mtoto anaroho ya uzinzi ambayo ndiyo chanzo cha mvuto huo.

Siku moja niliwahi msikia mtu aliyezini tunaita kumbaka mtoto mdogo sana akisema sijajiona mwenzenu sijui nini kimetokea hapana sijajiona mwenzenu!!! Kwani kuna mtu alimwelewa? Ni fimbo mangumi na kisha jela.

Baada ya kuja kujifunza hili somo na kuanza kuyaona kwa macho mambo haya ninayokufundisha nilianza kumuelewa yule mtu wa kipindi kileee aliyesema mwenzenu sijajiona.

Sasa rudi ukaangalie hako katoto kaliko bakwa kalivyo. Unashangaa kanamacho fulani hivi kama vile hichokitendo kilichofanyika kanaona kawaida tu. Katakusimulia kila kitu utafikiri mtu mzima.

Nakwambia ukweli watoto wanamna hiyo hasa wa kike wako wengi sana tena sana. Sikutishi nakwambia ukweli hasa katika kizazi hiki tulichonacho sasa. Ukizaa watoto hasa wa kike unahitaji kwa kweli kuowaombea sana adui anapenda sana kuwaingia na kuwachomekea roho hii.

Sikia mtoto akiwa na roho ya namna hii utamfundisha utamchapa utamuonya lakini wapi! Utamficha kwenye nyumba ya geti lakini ataruka tu kutafuta wanaume. Usishangae atazini mpaka na wakata nyasi wa nyumbani kwako au walinzi wa getini kwako mpaka unashangaa hii tamaa aliyonayo ni yanamna gani? Wazee atawadandia tuu.

Ukimpeleka shule usishangae ata waambikiza tena kwa haraka mno rafiki zake tabia ya uzinzi. Watu wa namna watu wengine wanasema yule binti anadamu kali au ana nyota kali yaani kila mwanaume anamfutia kimapenzi na akifuatwa tu hajui kusema hapa. Sikiliza hakuna cha damu kali ni roho ya uzinzi tu imemfunika. Ngoja nikuonyeshe mfano mwingine uone.

Angalia mistari hii. “Mikaya akasema, Kama BWANA aishivyo, neno lile BWANA aniambialo, ndilo nitakalolinena.Na alipokuja kwa mfalme, mfalme alimwambia, Je! Mikaya, tuende Ramoth-Gileadi kupiga vita, au tunyamaze? Akamwambia, Kwea, ufanikiwe; kwa kuwa BWANA atautia mkononi mwa mfalme. Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la BWANA? Akasema, Naliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Je! Sikukuambia, hatanibashiria mema, ila mabaya?Mikaya akasema, Sikia basi neno la BWANA; Nalimwona BWANA ameketi katika kiti chake cha enzi, na jeshi lote la mbinguni wamesimama upande wa mkono wake wa kuume na wa kushoto.BWANA akasema, Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili akwee Ramoth-Gileadi akaanguke? Basi huyu akasema hivi; na huyu hivi. Akatoka pepo, akasimama mbele za BWANA, akasema, Mimi nitamdanganya.BWANA akamwambia, Jinsi gani? Akasema, Nitaondoka, na kuwa pepo wa uongo kinywani mwa manabii wake wote. Akasema, Utamdanganya, na kudiriki pia; ondoka ukafanye hivyo. Basi angalia, BWANA ametia pepo wa uongo kinywani mwa manabii wako hawa wote; naye BWANA amenena mabaya juu yako.”(1Wafalme 22:14-23).

Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa pepo wa uongo  alipowaingia hao ndugu walijikuta wanasema uongo kabisaa.

Ukiutazama huo uongo utagundua haikua tabia yao ila ilikua ni tabia ya pepo wa uongo. Pepo huyo wa uongo alipowaingia hao manabii tu,wakajikuta wakilitumikia shauri la huyo pepo yasni wakasema uongo.

Bwana Yesu Kristo anapotupa agizo la kutoa mapepo alikua anajua kuwa kuna mambo mengi mabaya watu wanakutana nayo chanzo chake ni roho au mapepo au shetani.
Yanapotolewa tu hao watu hupokea uponyaji wa udhaifu mpaka tabia zao mbaya.
Ngoja nikuonyeshe mfano huu mwingine. ”Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao.”(Luka 22:3-4).

Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa chanzo cha tabia aliyoifanya Yuda ni shetani, shetani alipomuingia tu, akajikuta Yuda anayatenda yoote ayatakayo shetani. Ndiyo maana baadaye shetani alipomuacha Yuda  unaona Yuda anaingiwa na hali ya uchungu mkubwa mno kwa kile alichokifanya anakimbilia kujiua.

Ukilielewa somo hili utaona kwanini Yuda alifanya hivyo. Simuungi mkono kwa kujiua kwake. Ila nataka nikutazamishe uone hali aliyokua nayo baada ya mchochea tabia mbaya kuondoka Yuda alijishangaa sana ameisalitije damu ya mtu asiye na hatia?
Watu wengi wanafanya uzinzi kwa mfumo kama huo huo nakwambia. Wakimaliza kukifanya hilo tendo wengi hulia sana tuu, lakini kwakuwa hiyo bado imo ndani yao wanajikuta kila siku wakitenda uzinzi tuuu hata kama hawataki?

Naamini umeelewa sasa ninapokuambia tabia ya uzinzi inaweza kuwa inatokana na roho au pepo. Katika hatua inayofuata ntakufundisha namna ya kuitoa hiyo roho mwilini kama unaona kuwa huenda kuna roho ya namna hii ndani ya mwili wako.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

1. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org

2. YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).

3. Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika  “SOMA NENO LA MUNGU”

4. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”

5. DVDs 📀 au CDs 💿

6. VITABU.
NB: Wasiliana na Brigitha kwa namba +255 (0) 763 109 733, kupata VITABU, DVD & CD.

7. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

8. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:-  radio.mwakatwila.org

Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 (0) 754 849 924 Au +255 (0) 756 715 222

Wako
Mwl Steven & Beth Mwakatwila.
13/02/2019

No comments:

Post a Comment