8️⃣ MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE WOKOVU KATIKA ENEO LA MATATIZO YALETWAYO NA TAUNI
Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA.
FUATANA NASI:- KWENYE APP, FACEBOOK, INSTAGRAM, ONLINE RADIO 📻, WEBSITE, WHATSAPP & YOUTUBE Kwa links zilizoko hapa kwenye link hii:
KUPATA APP YETU “HUSONEMU (MWAKATWILA) APP”: (humo utapata masomo haya yote ninayokuletea darasani na mengine mengi) bonyeza link hapa.
🖊️ 06 /04/ 2020.
Bwana Yesu Kristo asifiwe. Ninakukaribisha tena darasani ili tupate kujifunza somo hili muhimu.
HIKI NI KIPINDI CHA NANE.
JAMBO LA NANE
H. JIFUNZE KUKIRI USHINDI KWA KINYWA CHAKO.
Mungu ili akuokoe katika majanga pia atataka kuangalia ukiri wako: “Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya. Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe. Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia. Mimi nayaumba matunda ya midomo; Amani, amani, kwake yeye aliye mbali, na kwake yeye aliye karibu; asema BWANA; nami nitamponya.” (Isaya 16-19)
Mungu anapokasirika na kuadhibu ili aponye fahamu ataangalia maneno yasemwayo.
Angalia vizuri anasema atamponya huyo aliyepinga na kumletea amani kwa sababu Mungu anayaumba matunda ya midomo.
ILI UTOLEWE KWENYE MAUTI LAZIMA UJIFUNZE KUKIRI HUO WOKOVU
Angalia hii mistari uone: “Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.” (Mithali 18:20-21)
Katika kipindi hiki unatakiwa ubadilike katika kusema kwako. Anza kukiri huo wokovu usiseme kwa kinywa chako kuwa utakufa.
Angalia mistari hii: “Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.” (Zaburi 118:17)
Ukitaka upone majanga haya nakushauri jifunze kuukiri wokovu kutoka kwa Mungu. Angalia mistari hii: “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!” (Warumi 10:10-15)
Naamini umenielewa mpendwa katika ujumbe huu ambao Roho Mtakatifu aliniwekea ndani ya moyo wangu na nikapata kibali cha kukushirikisha.
Mungu akubariki sana.
Tunapoachana nataka nikupe taarifa hii kuwa ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
1. App yetu ya huduma yenye jina “MWAKATWILA” utaipata Play Store kwenye link pale juu, ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
3. YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
4. Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya Facebook (f) "like" na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “steven-mwakatwila”
6. DVDs 📀 au CDs 💿
7. VITABU.
NB: Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 754 849 924 Au
+255 756 715 222
Wako
Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.
🖊️ 06/04/2020.
No comments:
Post a Comment