Tuesday, April 28, 2020

Salamu – Mei, 2019

Salamu – Mei, 2019 Nina wasalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo aliye hai. Tunamshukuru Mungu sana ambaye ametulinda na kutupatia mwezi huu wa tano. Ni neema kubwa. Nimekuletea tena salamu za mwezi wa tano. Kumbuka tuna salamu tunazotembea nazo zenye kichwa JIFUNZE KUISHI MAISHA YA UTAKASO Katika salamu za mwezi uliopita tulianza kujifunza eneo la JIFUNZE KUTAKASA KILA TENDO LILILOANDIKWA KATIKA VITABU VYA MATENDO MBINGUNI NA DUNIANI Na tuliangalia mistari hii. ” Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.”(Waebrania 9:22-23) Ebu tusogee mbele kidogo. FAHAMU MATENDO YAKO UYATENDAYO YAPO YANAYOKUTANGULIA MBINGUNI NA WENGINE YANAWAFUATIA Angalia mistari hii. “Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata.”(1Timotheo 5:24) Ukiisoma hiyo mistari utagundua kuwa dhambi inapofanywa na mtu, mtu huyo lazima ajue tendo hilo alilolifanya ovu litamtamgulia huko mbeleni. Atalikuta siku ile ya hukumu. Maana yake nini? Unaweza kupata maana nyingi tu, lakini moja ya maana ni hii ninayokuambia matendo ya mtu yanatunzwa huko mbinguni ambako ndiko sote tutaenda. Na matendo hayo unayoyafanya yanatunzwa kwa mtindo wa kuonekana yaani yanarekodiwa kama kwa video camera hivi. Biblia inasema siku ile ya mwisho matendo ya kila mtu yatakua dhahili. Angalia mistari hii. “Dhambi za watu wengine zi dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhambi zao zawafuata. Vivyo hivyo matendo yaliyo mazuri ya dhahiri; wala yale yasiyo dhahiri hayawezi kusitirika.”(1Timotheo 5:24-25) Neno dhahili maana yake ni wazi wazi. Ni kuonekana, sasa unaposikia matendo yao dhambi zao zimewatangulia na zipo dhahili maana yake siku ya hukumu kila mtu matendo yake mabaya aliyoyafanya atayakuta kwenye hizo nakala zilizotunzwa huko mbinguni Sikiliza kuna maeneo mawili yanayotunza kumbukumbu za matendo ya watu. Moja ni mbinguni mbili ni duniani. Unajua huku duniani fahamu kuna kumbukumbu za matendo yako. Kunadhambi zilizokutangulia zingine zinakufuata maana yake ni hivi. Kuna nakara zinazotunza taarifa zako ziko mbinguni ukifa utaenda kuzikuta na kuna zitakazo kufuata maana yake ni nakara zilizotunzwa duniani. Unapofanya toba lazima ujue kushughulikia hizo nakala za pande zote mbili. Ngoja nikutafakarishe kidogo. Si unajua unaweza ukawa una copy mbili zinazofanana? Kunautofauti wa nakala halisi nanakala kivuli. Biblia inasema wazi kuwa kuna mambo ya mbinguni yaliyodhahili na ya duniani ambayo nikivuli au copy ya mambo yaliyoko duniani. Angalia mistari hii. “Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao. Kama ndivyo, je! Dhabihu hazingekoma kutolewa; kwa maana waabuduo, wakiisha kusafishwa mara moja, wasingejiona tena kuwa na dhambi? Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka. Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.”(Waebrania 10:1-4). Ukiipitia hiyo mistari utagundua hiki ninachokufundisha. Damu ya mafahali au wanyama iliweza kushughulikia kufuta au kutakasa au kufunika matendo maovu yaliyofanywa na mtu huku duniani tu. Mbinguni walikua bado wakizitunza hizo kumbukumbu ingawa huku duniani zikiwa zimefutwa. Ninachotaka nikufundishe ni hiki. Jifunze kuomba maombi mara kwa mara kwa Mungu afute matendo yako mabaya yaliyoko kwenye nakala zote mbili. Yaani nakala za duniani ambazo zinaweza kukufuata, na nakala zilizoko mbinguni ambazo wewe zimekutangulia nawewe utazikuta huko mbinguni. Ebu tufuatane katika kona hii katika kipindi kijacho. Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo 1.Website yetu ya www.makatwila.org 2. Youtube- Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU 3.Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga 4.Dvds au Cd 5.Vitabu 6.Kwa njia ya Redio mbalimbali Rungwe fm102.5 Kila siku Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku na Baraka Fm107.5 kila siku ya jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku na Bomba fm 104.1 kila siku ya ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku 7: Unaweza kutupata kwenye redio yetu online ya. radio.mwakatwila.org Kwa mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi. 0754849924-0756715222 Wako Mr &Mrs Steven Mwakatwila

No comments:

Post a Comment