Tuesday, April 28, 2020

Salamu – Aprili, 2019

Salamu – Aprili, 2019 Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Naamini unaendelea vema. Nimekuletea mfululizo wa salama za mwezi. Kumbuka tunasalamu zenye kichwa .Ebu tusogee mbele kidogo j JIFUNZE KUISHI MAISHA YA UTAKASO JIFUNZE KUTAKASA KILA TENDO LILILOANDIKWA KATIKA VITABU VYA MATENDO MBINGUNI NA DUNIANI Sikiliza. Moja ya eneo ambalo unatakiwa ulijue na ulishughulikie ni hili la kufanya maombi mara kwa mara ya kuomba Mungu Roho Mtakatifu kwa kutumia Damu ya Bwana Yesu Kristo atakase matendo mafu au maovu ambayo yameandikwa au kutunzwa huko mbinguni. Biblia inatufundisha kuwa mbinguni kuna kazi ya kutunza kila matendo au maneno mabaya ambayo wanadamu wanayafanya na kuyasema. Angalia mistari hii. “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo.”(Waebrania 9:22-23). Angalia kitu hiki, mbinguni kuna nakara ambazo zinatakiwa zisafishwe kwa damu. Katika agano la kalenakala hizo zilikua haziwezi kusafishika kwasababu ya upungufu wa ubora wa damu za wanyama ambazo zilitumika kufanyia utakaso. Kwa masna nzuri iko hivi. Huku duniani Mungu aliamuru matendo mafu yoote yatakaswe kwa damu. Kitu cha kujifunza hapo ni hiki. Damu za wanyama zilizotumika kufanyia utakaso zilishindwa kufanyia utakaso wa nakara zilizotunzwa mbinguni za matendo hayo hayo mabaya yaliyofanywa na watu. Maandiko yanasema hivi. “ambayo ndiyo mfano wa wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zinatolewa, zisizoweza kwa jinsi ya dhambi kumkamilisha mtu aabuduye, kwa kuwa ni sheria za jinsi ya mwili tu, vyakula na vinywaji na kutawadha kwingine kwingine, zilizoamriwa hata wakati wa matengenezo mapya. Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?”(Waebrania 9:9-14). Ukiipitia hiyo mistari utaona damu za hao wanyama hazikua na nguvu za kusafisha kila kitu. Hazikufanikiwa kusafisha nakala za matendo mafu ambazo zilikua zikitunzwa mbinguni. Angalia mfano Biblia inasema “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo” Ebu tujiulize mbinguni kuna dhambi inayofanyika? Kama hakuna kwanini nakala zilizoko huko zisafishwe? Nini kilikua kikitunzwa humo kwenye hizo nakala? Sikiliza. Mbinguni wanatabia ya kutunzwa matendo yetu mbalimbali. Ndiyo maana unatakiwa ujifunze mno namna ya kujifanyia utakaso. Unaweza kujitakasa roho, nafsi, na mwili lakini usishughulikie nakala zilizo beba kumbukumbu ya matendo yako mafu ambazo zinatunzwa huko mbinguni. Naamini sasa umeanza kunielewa ninaposema jifunze kufanyia utakaso wa matendo yako mafu yaliyotunzwa mbinguni. Katika salamu za mwezi ujao tutaendelea kujifunza kiundani kidogo mahali hapohapo. Mungu akubariki tuonane katika sehemu hii mwezi ujao. Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo 1.Website yetu ya www.makatwila.org 2. Youtube- Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU 3.Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga 4.Dvds au Cd 5.Vitabu 6.Kwa njia ya Redio mbalimbali Rungwe fm102.5 Kila siku Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku na Baraka Fm107.5 kila siku ya jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku na Bomba fm 104.1 kila siku ya ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku 7: Unaweza kutupata kwenye redio yetu online ya. radio.mwakatwila.org Kwa mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi. 0754849924-0756715222 Wako Mr &Mrs Steven Mwakatwila

No comments:

Post a Comment