1⃣8⃣ MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI
Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA
FUATANA NASI:- APP, FACEBOOK, INSTAGRAM, ONLINE RADIO 📻, WHATSAPP, WEBSITE & YOUTUBE, Kwa links zilizoko kwenye HII LINK hapa:
KUPATA APP YETU “HUSONEMU (MWAKATWILA) APP” BONYEZA LINK HII HAPA:
🗓 21 Februari, 2019
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Tu amshukuru Mungu aliyetupa siku hii nyingine. Naamini kuwa kuna maarifa fulani Mungu Roho Mtakatifu amekuwa akikupa kupitia somo hili.
Hebu tuendelee mbele kidogo kumbuka ninakuonyesha eneo lile la njia ambazo roho mbaya au mapepo yanavyoweza kuzitumia katika kumwingia mtu.
Nia yangu ya kukuonyesha hizo njia nataka uhakikishe kwanza unaijua au kuifahamu milango hiyo ndiyo itakuwa rahisi kuifunga au kuyaondoa hayo mapepo.
Hebu tuone njia nyingine ambayo inaweza kuyafungulia mapepo mlango. Nayo ni hii.
KUJIUNGANISHA KWA NJIA YA UTOTO WA KIROHO
Ngoja nikuambie jambo gumu sana ambalo watu wengi hawalijui. Watu wengi wanapookoka wanakosa makuzi mazuri na kitendo hicho hupelekea watu hao kujikuta wakivamiwa na mapepo.
Biblia inazungumzia habari za kukua kwetu kiroho. “Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu; ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.” (1Petro 2:1-3).
Tunatakiwa tukue kiroho yaani ufahamu wetu wa mambo ya Mungu unatakiwa ukue. Unajua hatari ya mtu kutokukua ni hii. Hawezi kupambanua mambo mema na mambo mabaya.
Angalia mistari isemavyo “Ambaye tuna maneno mengi ya kunena katika habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia. Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu. Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga. Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.” (Waebrania 5:11-14).
Mtoto kiroho hawezi kupambanua ipi ni roho ya kweli na ipi ni roho ya mapepo. Kumbuka adui anaweza kuja kabisa kama malaika wa nuru. Kumbuka hili sana.
Maandiko yanatuonya kuwa “Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” (1 Yohana 4:1).
Sasa ukiwa mtoto kiroho ni ngumu sana kuitambua roho ya uongo au mapepo. Kwa sababu yanapokuja yanaweza kuja kwa njia nzuri kabisa ambayo mtoto kiroho kutambua ni ngumu mno.
Angalia mfano hapo tunaambiwa roho ya manabii wa uongo. Neno unabii maana yake ni neno lililotoka kwenye ulimwengu wa roho moja kwa moja si lililoandikwa. Mfano kutabiriwa au kutabiri ni tendo la kinabii.
Neno nabii ni ofisi au huduma maalumu ambayo mtu amepewa na Mungu au miungu (shetani). Sasa usifikiri nabii wa uongo atakutabiria mambo ambayo utayatambua haraka haraka kuwa ni ya uongo, inahitaji mtu mzima kiroho kupambanua ipi ni roho ya uongo na ipi ni roho ya kweli.
Unajua ni rahisi sana ukatambua mtu aliyebeba ujumbe unaomkana Bwana Yesu Kristo kuliko mtu ajaye akimkiri Bwana Yesu Kristo huku akiwa amebeba mapepo yaani roho ya uongo.
Lazima mtu awe amekua kiroho au ufahamu wake katika neno la Mungu uwe mkubwa.
Sasa kutokana na jambo hili utaona ni rahisi sana mtu akajikuta anajiunganisha au anaunganishwa na mapepo ya aina mbalimbali pasipo kujua kisa ni utoto tu alionao katika mambo ya Mungu.
Watu wengi wanapookoka wanajikuta ghafla wanaanza kuwa na kiu kubwa ya kumfahamu Mungu. Na wengi baada ya kumwamini tu Bwana Yesu Kristo wanaanza kutafuta kwa nguvu mawasiliano au ushirika na Mungu.
Wengine hujikuta wakitafuta kweli kutaka kumtumikia Mungu, wengine hutafuta haraka sana waondolewe taabu zao si wameokoka sasa wanaona kuwa na shida fulani fulani ni kama hawajaokoka vile huanza kwa bidii kutafuta msaada kutoka kwa Bwana Yesu Kristo ili watoke kwenye hizo shida zao mbalimbali.
Bahati mbaya kwa sababu ya utoto walionao ni rahisi sana wakajikuta wakinaswa kwenye huo mtego. Sikiliza kuumwa na kupata matatizo ni sehemu ya maisha kabisaa ya mtu anayemwamini Bwana Yesu Kristo.
Sasa usipokuwa mtulivu katika kipindi hicho cha utafutaji msaada wako nakuhakikishia kama ni mtoto kiroho utajikuta umeangukia kwenye hili ninalokuambia kabisaa.

Nakufundisha kitu muhimu mno, najua watu wengi hawataki kukisikia lakini wewe wafuatilie mwisho wao utagundua ninachokuambia.
Watu wengi wanapenda kuwekewa mikono na kuombewa na hata kutoa sadaka zao kila sehemu bila kujua madhara yake.
Ngoja nikuonyeshe kitu hiki. Mimi sibabaiki na uponyaji au miujiza au unabii au maombi ya baraka tele. Unaweza ukaniambia mtumishi nilikuwa naumwa nimepokea uponyaji, au maisha yangu yamebadilika kiuchumi au yaani kuna miujiza mikubwa nk.
Unaweza pokea uponyaji kabisaa au ukaona miujiza kabisaa na ukapokea unabii unaoonekana ni wa kweli kabisaa tena kwa jina la Bwana Yesu Kristo lakini huyo mtoa huo uponyaji asiwe Bwana Yesu Kristo kabisaa.
Maandiko yako wazi yanasema hivi “Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.” (Mathayo 7:22-23).
Fikiria kidogo hao watu Bwana Yesu Kristo anasema SIKUWAJUA NINYI KAMWE!!! Fikiria Bwana Yesu Kristo hawajui ila wanayafanya hayo wanayapata wapi?
Nakushauri tulia acha kuhangaika kwenda huku na huku labda uwe umekua kiroho na unajua kupambanua roho itendayo kazi ni ya nani.
⚠ Sikia wapo manabii, waalimu, Wachungaji, mitume na wainjilisti wa kweli kabisaa, lakini fahamu wapo pia watumishi wajao na sura hiyo lakini si watumishi wa Mungu aliye hai bali ni watumishi wa uongo wana roho mbaya ndani yao.
Ngoja nikuonyeshe mfano mwingine labda utanielewa ninavyokuambia usipokua kiroho ni hatari na unaweza kujikuta unajiambatanisha na mapepo.
Angalia mistari hii “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani; kwa unafiki wa watu wasemao uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli. Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba. Uwakumbushe ndugu mambo hayo, nawe utakuwa mtumishi mwema wa Kristo Yesu, na mzoevu wa maneno ya imani, na mafundisho mazuri yale uliyoyafuata.” (1 Timotheo 4:1-6).
Angalia pia mistari hii. “Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” (Yohana 6:63).
Ukiisoma hiyo mistari katika kitabu cha Timotheo utaona tunaambiwa kuna watu watasikikiza mafundisho ya mashetani au roho zidanganyazo, maana yake kuna maneno ambayo shetani atayaachilia tena ndani ya watu waliookoka kabisa.
Fahamu mafundisho hayo ni maneno. Na tunaambiwa katika kitabu cha Yohana kuwa maneno tunayoambiwa na Bwana Yesu Kristo ndiyo roho. Sasa angalia mtu akisikiliza maneno yaliyotoka kwa nabii wa uongo au mwalimu wa uongo, nk ataipokea roho mbaya.
Unaweza kujiuliza ataipokeaje? sikiliza MANENO TUAMBIAYO NDIYO ROHO!!!!
Unapopokea utabiri wa kutoka kwa shetani aliyekuja kama nabii wa Mungu fahamu unapomsikiliza na unapomwamini tu kwa kuanza kuyatenda hayo unapokea roho mbaya iliyobebwa katika hilo neno ulililolisiki na ukaliamini.
Watu wengi hupenda kusikia tuuu na hawapimi hilo wasikialo yaani hatari yake ni kupokea mapepo tu. Na huwezi kupima ukiwa mtoto.
Ushauri wangu kwa nini usifanye maamuzi ya kutafuta kukua kwanza kuliko kutafuta hiyo miujiza unabii na hata mafundisho magumu ambayo umri wako wa kiroho bado sana kuyafikia?
Ngoja nikupe mfano huu uone. Angalia, watu wengi ni watoto kiroho wanataka kufunga siku arobaini, ishirini nk. Mimi hainipi shida wewe kufunga, shida yangu iko hapa hivi unajua ufungapo siku nyingi na kuomba sanaa na huku ukiwa mtoto kiroho hatari yake unaweza kukutana na shetani na akakushinda tu kwa sababu ni mtoto tu kiroho?
Angalia mistari hii “Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani, akijaribiwa na Ibilisi. Na siku hizo alikuwa hali kitu; hata zilipotimia, aliona njaa. Ibilisi akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, liambie jiwe hili liwe mkate. Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo. Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Akamwongoza mpaka Yerusalemu, akamweka juu ya kinara cha hekalu, akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini;kwa maana imeandikwa, Atakuagizia malaika zake wakulinde; na ya kwamba, Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe. Yesu akajibu akamwambia, Imenenwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako. Basi alipomaliza kila jaribu, Ibilisi akamwacha akaenda zake kwa muda. Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.” (Luka 4:1-14).
Ukipitia hiyo mistari utagundua hiki ninachokufundisha. Watu wengi wana haraka kweli, hawajajaa Roho Mtakatifu bado, hawana nguvu za Roho Mtakatifu bado hawana neno la Mungu la kutosha wanaanza kufunga siku arobaini nk.
Hawajui kuwa wanapoifanya huduma ya namna hiyo wanaweza kukutana na mapepo na yakaja kama hivyo na yakawavuruga kweli kweli.
Wewe watazame wengi wanajikurupukia katika kuyafanya hayo mapema mnoo kabla ya kukaa chini ya miguu ya Bwana Yesu Kristo awafundishe mambo mengi ndipo waongozwe na Roho Mtakatifu kuyafanya hayo.
Ngoja nikuulize swali umewaona akina Petro wanafunga siku hizo arobaini walipokutana tu na Bwana Yesu Kristo? Wanafunzi wa Yohana waligundua kuwa wanafunzi wa Bwana Yesu Kristo hawafungi, na Bwana Yesu Kristo hakukataa, alikubali kuwa hao ndugu hawafungi.
Kwa nini walikuwa hawafungi kipindi hicho? Fahamu walikuwa watoto, walihitaji kwanza wakae shule wapigwe elimu mbalimbali ndipo waanze kufunga.
Fikiria kidogo mtu ameokoka ana siku mbili tu, anafundishwa aanze kufanya maombi ya vita, abomoe madhabahu za mababu na mabibi, ateke eneo lililokaliwa na ibilisi miaka zaidi ya mia mbili wewe unafikiria kweli huyo mtu atakosa kuvamiwa na mapepo?
Umewahi kujiuliza swali kwa nini Bwana Yesu alikaa na wanafunzi miaka mitatu? Sema alikuwa anawakuza kiroho. Fikiria Mwalimu Mkuu wetu anakaa na watu uso kwa uso miaka mitatu akiwapiga shule, na bado aliwaonya wasitoke kwenda huko kushuhudia na kuhubiri mpaka wajazwe nguvu na Roho Mtakatifu.
Leo hii mtu anaokoka siku nne tu tunamtwisha mzigo wa kuomba lisaa limoja, na kumpa kumtolea unabii wa mafanikio wakati hata njia za hayo mafanikio hatujampatia si kesho ukisikia anauza uyoga wa kichina na madumu ya alovela na kubet sijui kesho ana majani kutoka nchi gani eti yanatibu kisukari yaani ukitulia utaona namna watoto wa Mungu walivyowaganga wa kienyeji.
Ngoja nikuchekeshe kuna kipindi nililetewa majani fulani ya chai, nikaambiwa yanatoka nchi moja ya Asia. Kweli nilitumia. Siku moja nikaona ono nimepelekwa hiyo nchi, niliyoyaona wewe acha tu. Nikamwuliza Roho Mtakatifu nini maana ya maono hayo?
Mungu akaniambia acha kutumia hayo majani ya chai. Nikamwambia mke wangu. Tukaacha kutumia niliona mapepo tu. Sasa mimi niliombea nikanywa Mungu akanishitua, wewe wafuatilie watu wanaojiingiza kwenye hizo biashara utagundua wengi wameingiliwa na roho za ajabu ajabu, wengine ghafla wamekuwa wazinzi hawajui hata hiyo tabia ya uzinzi imeanzia wapi.
Ngoja nikupe mfano huu. Siku moja Mungu alinionyesha ono, alinichukua nilipokuwa akanipeleka kwa baba yangu mzazi, nikamwona baba yangu akiwa na mtu mmoja amevaa mavazi kama daktari hivi mpaka kile kifaa cha kupimia wagonjwa.
Nikaona anampa baba yangu vidonge akisema nenda kampe atapona kabisa ugonjwa wa moyo na kisukari. Cha ajabu Mungu akanifunulia huyo mtu niliona ni mchawi tu yaani mganga wa kienyeji.
Roho Mtakatifu akaniambia nenda kamkataze baba yako asimpe mama yako hiyo dawa. Nikaondoka mpaka nyumbani kwetu. Kweli nilipoongea na baba akasema amepewa hiyo dawa ili ampe mama kwa ajili ya BP na eti hiyo dawa inatibu pia kisukari.
Nilipomfuatilia huyo mtu aliyempa niligundua ameokoka na anafanya kazi hospitali kubwa tu anayapeleka madawa yake huko ili yafanyiwe utafiti. Na baada ya siku si nyingi nilimkuta akiizindika nyumba ya mtu mmoja ambaye alimpangisha mfanyakazi mwenzetu.
Yule mfanyakazi aliwahi kuniambia kuwa anapoishi mwenye nyumba humleta mganga mara kwa mara sasa bahati nzuri siku hiyo nilienda kumtembelea huyo ndugu mwenye nyumba akamleta huyo mganga.
Yule ndugu alipomwona huyo mganga akiizindika nyumba kubwa kwanza kabla hajaja kwenye nyumba ndogo aliompangisha huyo ndugu yangu, akaniambia mtumishi yule mganga niliyekuwa nakuambia leo kaja sijui unafanyaje hapa?
Nikaomba Roho Mtakatifu atuvushe hapo salama, fikiria mimi nimo ndani ya nyumba iliyo zamu ya kuzindikwa!!! Nikapewa akili ya kutoka nje na kumfuata mwenye nyumba na mganga wake huko huko.
Nilipotoka nje aisee kuja kumwona mganga ni mtu ninayemfahamu tena anajiita mtumishi na daktari mtafiti!! Unajua aliponiona tu. Ehehehee aliacha kazi iliyomleta mwenye nyumba akabaki ananishangaa tu. Lilikuwa bonge la fumanizi!!!
Huwa najiuliza hivi watu aliowawekea mikono akiwaombea tena kwa jina la Bwana Yesu Kristo walipokea roho gani?
Nimewaona watu wengi sana wakijikuta leo hii wana maono ya kuacha wake zao au waume zao wengine utawakuta wanaona kila mtu ni mchawi utasikia naomba maombi mtumishi unamwuliza nikuombee nini utasikia baba yangu ni mchawi au mama yake ni mchawi.
Yaani utakuta familia nzima imeingia kwenye ugomvi mkubwa mnoo. Unamwuliza umejuaje kuwa baba yako au mama yako au mkeo ni mchawi? Utasikia ni nabii ameniambia.
Mwingine utasikia tulikuwa kwenye maombi ya kukemea pepo na ndipo limetuambia kuwa baba au mama au mke au mtumishi fulani ni mchawi!! Na ameamini kweli, ukiona hivyo fahamu wamesikia roho ya uongo na wameiamini na tayari ushirika wao na mapepo ni mkubwa mno.
Usishagae sana tabia zao zinaanza kubadilika taratibu, wengine utawaona wanaanza kuwa na chuki na watu fulani, wanaanza kuwachukia na kujitenga na watu, ndugu na wengine unaona kabisa hata kazi wanaacha usishangae utamwona anaanza kuhukumu watu weee, yaani ghafla utamwona binti anaanza kuwa bibi taratibu, haogi hachani nywele kesho kutwa usione ajabu utamkuta kachoma suti zake zoote au nguo kisa nabii kamwambia hizo nguo ni za mapepo.
Yaani utoto kiroho ni hatari sana. Nakushauri jifunze kutulia. Usipende kuwekewa mikono na kila mtumishi, usipende kutabiriwa ovyo ovyo si kila mtu ajiitaye au anayeitwa nabii ni nabii wa kweli hata kama anayajua mambo mengi mnoo yakuhusuyo adui anaweza kutambua kabisa.
Soma Biblia wewe mwenyewe, sikiliza kila mafundisho au soma kila kitabu lakini usikurupuke kuyaweka kwenye matendo hayo uliojifunza kwanza yaangalie maandiko yanasemaje juu ya hilo.
Ondoa uvivu wa kusoma Biblia wewe mwenyewe. Pia angalia umebandikwa mikono na watumishi wa aina gani! Sikiliza mtumishi mzinzi akikuwekea mikono ni rahisi roho ya uzinzi kukuvaa wewe.
Naamini umenielewa

Mungu akubariki sana.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
1. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
2. YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
3. Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
4. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
5. DVDs 📀 au CDs 💿
6. VITABU.
NB: Wasiliana na Brigitha kwa namba +255 (0) 763 109 733, kupata VITABU, DVD & CD.
7. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 (0) 754 849 924 Au +255 (0) 756 715 222
Wako
Mwl Steven & Beth Mwakatwila.
21/02/2019
No comments:
Post a Comment