Salamu – Agosti, 2019
Ninakusalimu ndugu yangu mpendwa. Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!! Pole na kazi zoote ambazo umekuwa nazo katika mwezi uliopita. Na nikupe pole ya magumu yoyote ambayo umekutana nayo katika mwezi huo.
Binafsi katika mwezi uliopita, tumekuwa na semina Chimala tulifunga hema pale, tukawa na Semina Jijini Mbeya katika kanisa la KKKT Uyole. Na tukaelekea Arusha katika Conference ya watumishi kutoka nchi mbalimbali.
Kwa kweli mwezi huo tumemwona sana Mungu akitutunza kutulinda na kutupigania. Nimekuletea salamu za mwezi.
Hebu tusogee mbele kidogo.
JIFUNZE KUMWOMBA ROHO MTAKATIFU ASHUGHULIKIE HIZO NAKALA
Sikiliza, nilikufundisha kuwaili nakala za mbinguni zilizobeba kumbukumbu za mabaya yako wewe zifutwe ni lazima ujifunze kutumia damu ya Bwana Yesu Kristo.
Na ili ushughulikie hizo nakala jifunze kuomba. Na unapoomba jifunze kumuomba Roho Mtakatifu azitakase hizo nakala. Angalia mistari hii: “Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?” (Waebrania 9:13-14)
Angalia na mistari hii: “Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake;” (Waebrania 2:11)
Ukiipitia hiyo mistari utaona Roho Mtakatifu ndiye anayetakasa. Huyu ndiye unatakiwa umwombe azitakase hizo nakala, kwa kutumia damu ya Bwana Yesu Kristo.
Katika maombi yako jifunze kumwomba afanye hivyo.
Mfano anza kuomba hivi. Tumia jina la Bwana Yesu Kristo katika hayo maombi, Tubia dhambi zako zoote, anza kumwomba Roho Mtakatifu akutakase kwa kutumia damu ya Bwana Yesu Kristo na maji yaliyotoka ubavuni mwa Bwana Yesu Kristo kujitakasa. Mwambie akutakase, roho, nafsi au moyo na mwili.
Omba pia ashughulikie hizo nakala zoote zilizoandikwa matendo yako mabaya. Roho Mtakatifu ndiye msaidizi wetu. Kaletwa kwetu ili kutusaidia.
Yupo tayari kutusaidia katika eneo hili la kujitaka kwa kuzifuta nakala za vitu vya mbinguni.
Kama unaweza kuomba kwa Roho yaani kunena kwa Lugha hiyo itakuwa vizuri sana. Unaanza kuomba akili au kikawaida halafu jiruhusu kuanza kunena.
Ukisikia huzuni na ukataka kulia usisite wewe lia hata kama hujui unalilia nini. Roho Mtakatifu anaweza kuugua huko ndani na kulia sana ili ufutiwe mabaya yako mpendwa.
Basi wewe lia kama unajisikia kulia unavyoomba maombi ya mvumo huu kwa ajili yako au kwa ajili ya watu wengine
Kama huna uwezo wa kunena kwa lugha usiogope, wewe omba kwa akili au kawaida. Ukisikia kulia pia lia tu.
Mwombe Roho Mtakatifu akufutie hata hayo matendo mabaya yanayokufuatia. Omba kila siku maombi ya namna hii.
Unaweza kuomba kwa sauti kubwa au ya kati au ndogo au kimoyomoyo. Fahamu Mungu atasikia tu.
Hebu sasa anza kuomba na iwe sehemu ya maisha yako ya kuyaomba maombi ya mfumo huo.
Mungu akubariki sana. Tuonane katika kona hii mwezi ujao.
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo;
1. App yetu ya huduma yenye jina “HUSONEMU (MWAKATWILA)” utaipata Play Store kwenye link pale juu, ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
3. YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
4. Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya Facebook (f) "like" na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
6. DVDs 📀 au CDs 💿
7. VITABU.
NB: Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
9. Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 754 849 924 Au
+255 756 715 222
Wako
Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.
No comments:
Post a Comment