Salamu – Disemba, 2019
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana sana, Huu ni mwisho wa Mwaka, ni mwezi muhimu sana na ni neema kubwa kuufikia.
Tunapaswa kumshukuru Mungu mnoo. Katika mwezi uliopita tumekuwa na semina Mafinga tulifunga hema na tukaelekea Makambako tulikuwa na semina ya ndoa na tukaenda Ubaruku huko tulifunga hema.
Tulikuwa na semina nzuri sana. Hebu tumalizie leo salamu za mwezi ambazo tumekuwa nazo karibu miaka miwili. Yaani mwaka jana na mwaka huu tumekuwa tukijifunza somo lenye kichwa:
JIFUNZE KUISHI MAISHA YA UTAKASO
Hizi ni salamu za mwisho, mwakani tutaanza kupokea salamu mpya za kila mwezi kwenye eneo hili la salamu za mwezi.
Hebu tuendelee mbele kidogo.
JIFUNZE PIA KUITAKASA MADHABAHU
Unaposoma Biblia eneo jingine linalotakiwa tulitakase ni madhabahu. Madhabahu ilikuwa ikikaa ndani ya hema. Na ilitengenezewa na yenyewe utaratibu wa namna ya kuitakasa.
Angalia mistari hii uone: “Kila siku utamtoa ng’ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa. Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.” (Kutoka 29:36-37)
Mungu anatufundisha hapo kuwa, hema ilitakiwa itakaswe na madhabahu pia ilitakiwa itakaswe. Biblia inasema madhabahu ilitakiwa ifanyiwe upatanisho na Mungu kwa muda wa siku saba.
Jiulize swali kwa nini madhabahu ya Mungu ifanyiwe upatanisho? Madhabahu hiyo fahamu ilikuwa ina kasoro nyingi tu. Mungu hawezi kusema nipatanishe na madhabahu kama hakuna ugomvi kati ya Mungu na hiyo madhabahu.
Madhabahu ilitakaswa maana yake ilikuwa si safi. Ilitakaswa kwa mafuta na pia damu. Kuna mambo muhimu ambayo unaweza kuyafanya ili kuitakasa madhabahu.
MAOMBI YA UPATANISHO KATI YA MUNGU NA MADHABAHU
Lazima ujifunze kuomba maombi ya namna hii. Mwombe Mungu ajiunganishe au apatane na hiyo madhabahu kwa lugha nzuri airidhie. Ipatanishe kwa damu. “Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.” (Kutoka 8:15)
Tumia mafuta yaani ROHO MTAKATIFU KATIKA KUIFANYIA UTAKASO HIYO MADHABAHU. Angalia mistari hii: “Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.” (1 Yohana 2:27) Mafuta hayo ni Roho Mtakatifu. Anayeweza kutufundisha yoote na ndiye mafuta leo.
3: TUMIA DAMU YA BWANA YESU KRISTO KUITAKASA
“Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.” (Kutoka 8:15)
Angalia na mistari hii: “Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote.” (Kutoka 8:24)
Tumia maombi katika kuitakasa hiyo madhabahu kwa damu na kwa hayo mafuta na jifunze kumsikiliza sana Roho Mtakatifu anataka nini katika kuitakasa hiyo madhabahu na kuijenga.
4: JIFUNZE KUIWEKA SAFI HIYO MADHABAHU
Jifunze kuijenga madhabahu ya Mungu kwa ubora mpendwa. Na muiweke kuwa safi katika kila kitu. Kuanzia vitambaa, kapeti, na kila kitu kitakachokuwepo kiwe kisafi na kilicho bora.
Mimi Mungu alinionyesha zamani madhabahu anayotaka niitengeneze. Hii niliyonayo ndiyo picha niliyoiona niliona safi sana. Imewekwa juu yake maua na ilikuwa ndani ya hema. Na viti vilipangwa humo ndani vizuri uwanjani. Miaka hiyo mimi sijui hata kama nitakuwa hivi leo. Akaniambia nataka watu woote wakae humo ndani.
Ukiipitia hiyo mistari utajifunza kuwa tunahitaji kuishi maisha ya utakaso sana.
Naamini umepokea kitu katika somo hili. Mungu akubariki sana na tunaliandaa somo hili kama kitabu. Tuombee.
Asante kwa kunisikiliza Mungu akupe nafasi nyingine ya kuuona mwaka ujao wa 2020.
BARIKIWA SANA
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo;
1. App yetu ya huduma yenye jina “HUSONEMU (MWAKATWILA)” utaipata Play Store kwenye link pale juu, ambapo kuna masomo mengi sana hapo.
2. Tovuti yetu ya www.mwakatwila.org
3. YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
4. Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya Facebook (f) "like" na utapata maelezo ya kujiunga au ingia Facebook halafu andika “SOMA NENO LA MUNGU”
5. Instagram ingia Instagram app halafu andika “Steven Mwakatwila”
6. DVDs 📀 au CDs 💿
7. VITABU.
NB: Wasiliana na mhudumu ofisini kwa namba +255 763 109 733, ili kupata VITABU, DVD & CD.
8. Kwa njia ya REDIO:- Utapata mafundisho yetu kwa redio zifuatazo:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
Kwa Mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:-
+255 754 849 924 Au
+255 756 715 222
Wako
Mwl Mr & Mrs Steven Mwakatwila.
No comments:
Post a Comment