6⃣ MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI
Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA
FUATANA NASI FACEBOOK
FUATANA NASI YOUTUBE
FUATANA NASI ONLINE RADIO
👉🏼 radio.mwakatwila.org
22 Dec, 2018
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana, mimi na familia yangu ni wazima tunamshukuru Mungu. Ninakuletea tena somo hili kama mfululizo wa somo nililokuahidi kuwa nitakufundisha ili upate kujua nini cha kufanya na uanze kuishinda dhambi ya uzinzi.

Hebu tuendelee tena kidogo kuona namna unavyoweza kuishinda tabia ya uzinzi inayoletwa na chanzo cha mwili.
JIFUNZE KUIKIMBIA ZINAA USIJARIBU KUIPINGA
Sikiliza moja ya jambo lingine ambalo leo hii linaweza kuwa chanzo cha uzinzi kwa watu wengi ni hili la wao kujiamini kupitiliza katika eneo la kukabiliana na zinaa.
Watu wengi wameangushwa na zinaa ni kwa sababu ya wao kufikiri wataipinga wakati Biblia inasema ikimbieni. “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 6:18).
Umeyasikia hayo maneno mpendwa? Zinaa inakimbiwa, usijaribu kufikiria kuwa utaishinda kwa kujiamini. Ngoja nikuambie jambo kwa uzuri. Watu wengi hawachukui tahadhari kubwa katika hili suala.
Wapendwa au Wakristo wa kizazi cha sasa wanaishi maisha ya kwenye TV, hawataki kuishi maisha halisi ya kwenye Biblia, Maisha hayo wakiyaona ya wachumba wakikaa pamoja, wakikumbatiana na kubusiana, wanafikiri ni maisha halisia kumbe ya kuigiza.
Unatakiwa ujifunze kuchukua tahadhari kubwa mno unapokuwa na mtu wa jinsia tofauti na wewe. Iwe ofisini au nyumbani kwako nk. Ukikaa na mtu wa jinsia tofauti na wewe kwenye mazingira hatarishi kwa kujiamini nakuhakikishia usishangae mkajikuta mwili umewashinda tu.
Watu wengi wanapokuwa katika mahusiano maalumu ya kutakakuoana hapo ndipo hujikuta kwenye mtengo mkubwa wa mwili, watataka kuishi kama Wakristo wa kizazi kipya kwa kujiachia na kukutana maeneo yenye kuwatengenezea ukaribu uwajengeao ushawishi mkubwa wa kufanya zinaa na wengi huangukia hapo.
Usijaribu kujidanganya kuwa nitaishinda hiyo dhambi, unachotakiwa kukifanya ni kuikimbia kwa kujitengenezea mazingira salama. Fikiria kidogo unakubali kukaa chumbani kwa huyo usemaye atakuoa mkiwa wawili na huku mkitazamana kwa kutamaniana unasema nitaipinga hiyo dhambi?
Jifunze kuyakimbia mazingira yote ambayo utayaona ni hatari, fikiria kidogo eti wewe na mchumba wako mnaenda kuongelea mazungumzo yenu fukweni mwa bahari mko wawili! Mmoja anamwambia mwenziwe ngoja tukaoge eti!!!
Fikiria eti wewe unakaa na binti usiku unadai unamfundisha Biblia, eheheehe!! Nakuambia una muda mchache tu, utaanguka na huyo binti au kijana. Usijiachie kwa namna hiyo, mimi sikatai kuongea na msichana au mvulana, lakini mnaongelea wapi?
Fikiria namna Tamari alivyokosea na akaanguka “Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu kwake.Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake. Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.” (2 Samweli 13:8-19)
Ukiipitia hiyo mistari utagundua hiki ninachokisema, Tamari hakuchukua tahadhari ya kuikimbia zinaa. Angalia, Tamari anaona watu wanafukuzwa yeye hashituki tu, anaambiwa lete chakula, lete hapa, karibia hapa, anakwenda tu, haikimbii.
Angalia Yusufu alivyofanya, alikimbia, kama angejidanganya kubaki pale akijidai kuikemea hiyo dhambi nakuhakikishia angezini na yule mama. Mimi nakuambia ukweli angebaki pale nakuambia leo tungekuwa na habari nyingine.
Angalia mistari hii uone alichosema Yusufu. “Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu. Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri. Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami. Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu? Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.” (Mwanzo 39:6-12).
Unapoisoma hiyo mistari utaona kuna mambo mengi sana ambayo Yusufu aliyafanya na akajikuta anaikwepa dhambi ya uzinzi.
Jambo la kwanza, hakutaka kuzungumza au kuongea na huyo mwanamke, angalia Neno linasema hivi. “Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.”
Yusufu aliyakimbia mazungumzo kati yake na huyo mama, angalia kwa makini, huyo mama hakumshitukizia Yusufu, alianza muda mrefu kumtaka Yusufu. Kilichomsaidia Yusufu ni namna alivyokuwa anamkimbia huyo mama katika eneo la kukaa na kuzungumza.
Fikiria sana, Yusufu alikuwa mtumwa hapo, lakini alimkimbia huyo kwenye eneo la mazungumzo, alikuwa mjanja mno hapo. Moja ya jambo ambalo unatakiwa ulikimbie ni hili la mazungumzo au kujiachia kuongea na mtu akutakaye.
Jambo la pili naona Yusufu aliamua kumkimbia huyo mama alipomfuma mahali au kwenye eneo linaloonekana salama kwa kufanya dhambi, yaani walikuwa wawili tu. Ukiona upo na mtu wa jinsia tofauti kwenye mazingira ya namna hii na haujautazama mlango wa kutokea fahamu nakuambia utazini tu.
Nakumbuka miaka ile mimi sijaokoka pale mjini nilipokuwa naishi kulikuwa na binti mmoja nzuri kweli kweli wa umbo na sura. Mtoto mtoto kweli ehehee!!!! Siku hiyo mimi nilikuwa dukani kwa rafiki yangu muda wa saa tano hivi. Ghafla yule rafiki yangu akaniambia Steven, unaitwa hapo nje, nilipogeuka nikamwona huyo dada.
Nikataka kukataa kumfuata, rafiki zangu hapo dukani wakasema wote kwa pamoja, acha ujinga wewe nenda!!! Mwingine akasema hiyo ni bahati nisiichezee. Nikaenda kwa kujivutavuta.
Sikuwa na mazoea naye, ingawa wadogo zangu walikuwa na urafiki na huyo dada na familia yake. Mama yake nilikuwa namweshimu sana na alikuwa ni kiongozi mkubwa serikalini.
Walikuwa na maisha mazuri sana tu kwa kipindi kile tunakua. Nilipomwendea yule binti nilimkuta ana kapu kubwa jipyaa, katoka sokoni, sasa humo kajaza matunda, mboga na vitu vingi sana.
Akaniambia shika huko nisaidie kubeba. Nikamsikiliza, tukaondoka,hapo hatusemi. Kila mtu kimya. Tukafika mbali kidogo, nikamwambia kwanini uliamua kubeba kapu kubwa hili wakati huna mtu wa kukusaidia kulibeba akasema wewe utanisaidia mpaka nyumbani.
Nikasema sawa. Kweli tukafika nyumbani kwao. Akanikaribisha sebuleni, alikuwa na wadogo zake wawili, mmoja akamtuma aende kumpelekea bibi yake kitu. Ni mbali, huyo mwingine pia akamtuma. Akanipa soda, sasa miaka ile kuipata soda, wewe acha tu.
Nikaanza kuinywa taratibu, kwa kweli sikuwa na hisia yoyote ya kile anachotaka huyo dada, nilijiona sina hadhi ya kupendwa naye. Sasa sikia, Alipoondoka huyo mdogo wake wa mwisho, akatoka nikasikia anafunga mlango wa nyumba yao wa nyuma, akaja sebuleni, akatoka nje,akachungulia kama kuna mtu anakuja hivi.
Akajiridhisha kuwa hakuna mtu, akaufunga mlango kwa funguo. Anitazama kwa macho ambayo yalinipa taarifa haraka kuwa huyu dada kanipenda, akaja nilipokaa mimi na ubwege wangu, akafika akaniambia, Steven mimi siku zote nilikuwa nakupenda sasa leo nimefurahi umekuja kwetu tupo wawili usiogope mama hayupo.
Ngoja nikuchekeshe kidogo, Alipokuja pale, alivaa nguo ambayo tumbo lake likawa wazi sana, kwa mara ya kwanza ndiyo naona ile mistari ya wadada wanene, naamini umenielewa. Mimi ile mistari ilinishitua, nikafikiri huu siyo UKIMWI HUU!!!
Eheheeee!!! Nikajipanga haraka kumkimbia, haraka sana nikapata akili, wakati kanikumbatia, nikasema hivi kwa upole tu, “Ohoo kumbe unanipenda, hata mimi nakupenda, sasa sikia, hapa ni nyumbani kwenu. Kwa nini usije nyumbani kwangu? Hapa hapafai muda wowote mtu atafika hapa.”

Unajua akakubali kirahisi sana, akitaka tuondoke muda huo. Nikamdanganya kuwa, “njoo muda wa saa tisa, nina shughuli fulani mjini nikiimaliza muda huo nitamsubiri nyumbani kwangu.”
Akakubali, unajua nilipotoka pale ni mbio. Nilirudi nyumbani kwangu kwenye saa tano hivi usiku, unajua kila nikimwona nilikuwa natafuta njia ya kuchepukia nilimkimbia. Baada ya muda mrefu nilikutana naye, alinitazama tu wala hakusema alinidharau kweli.
Habari hiyo sikumwambia rafiki yangu yeyote kwani naona wangenicheka mpaka waanguke chini. Kwa kweli Mungu aliniokoa kweli Nilikimbia.
Mfalme Daudi alizini kwasababu hii hii ninayokuambia. Angalia mistari hii. “Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti? Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake. Yule mwanamke akachukua mimba; basi akapeleka na kumwambia Daudi, akasema, Ni mja-mzito. Ndipo Daudi akapeleka kwa Yoabu, akisema, Unipelekee Uria, Mhiti. Naye Yoabu akampeleka Uria kwa Daudi.” (2 Samweli 11:2-6).
Angalia hapo, mfalme Daudi alijiendekeza kutazama weee badala ya kukimbia. Mfalme Daudi alikuwa shujaa mno, lakini kitendo cha yeye kukaa kwa muda mrefu akimwangalia huyo mwanamke kiliuondoa ushujaa wote.
Wewe unaona kabisa huyu mtu ni kama ananitaka vile anakuandikia ujumbe unajibu, anaandika ujumbe wa pili unajibu, kadiri unavyofungua mlango wa kuongea naye ndivyo anatiririka kukuambia maneno mengi kwa nini usikimbie kwa kutomjibu?
Sikiliza usipojifunza kuikimbia zinaa nakuambia utajikuta umebanwa tu. Unapofungua mlango wa mazungumzo fahamu ni rahisi kubanwa. Fikiria unapokea zawadi kutoka kijana unazipokea weee, Jifunze kuikimbia zinaa nakuambia hizo zawadi au vichipsi hivyo, au unakubali mtu anasema leo tutoke tupate chakula cha mchana unakwenda badala ya kukimbia utajikuta unaanguka tu.
Wewe unaenda kwa mtumishi eti mmekaa wawili chumbani eti anakuombea ili ufunguliwe, unamruhusu akushike kila mahali eti anakuhudumia, sikia mtumishi wa namna hiyo mkimbie. Kimbia kabisaa, mwache, usiwe mjinga ukafikiria eti atakuombea maombi magumu au kukutenga.
Bora utengwe na mtumishi kuliko kutengwa na Mungu. Umemsikia Yusufu alivyosema, alisema hivi. “Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?” Jiulize nani wa kumkosa, Mungu au huyu mtumishi mzinzi tu?
Jifunze kuikimbia zinaa usikubali mtu anakuzoea haraka na mpaka anafika mwilini mwako wewe upo upo tu, fikiria mtu anakuomba namba ya simu hushituki tu, unampa akianza kukusumbua unaanza kulaumu kwa nini umpe namba zako za simu ovyo ovyo tuu.
Najua mabinti wengi wa sasa niseme neno gumu sana WAO NDIO CHANZO CHA KUFUATWAFUATWA. Wanajirahisisha mnoo. Unamchekea chekea mkaka kisa eti amekubariki kwenye huduma yake ya uimbaji. Unamkuta mbaba yuko vivyo hivyo. Anaona binti wa kazi kamkalia vibaya anajisemesha moyoni huyu mtoto sijui vipi. Wewe ikimbie dhambi, MWAMBIE KWA SAUTI TU WEWE KAA VIZURI NENDA KACHUKUE KANGA USINIKALIE UCHI HAPA!!!!
Unamkuta mtu ndiyo bosi ofisini hapo, eti anaona kabisaa anaona mmoja wa wafanyakazi tena usishangae ndiye katibu wake anamvalia nguo nusu uchi, anabaki kukemea tuu moyoni eti toka shetani ushindweee!!! Ehehee uzinzi unakimbiwa mpendwa.
Mwambie hapa ofisini siyo ufukweni, hatujaja kuogelea hapa, hapa ni ofisini hebu mavazi yawe ya heshima. Mimi nakuambia ukweli watu wengi wameanguka na hao waitwao maPS ehehee. Kisa ni hiki hiki.
Unamkuta mchungaji ndiyo anashindwa hata kuhubiri kisa eti mwanamke kakaa vibaya na yeye yupo juu madhabahuni. Sikia mwite mhudumu wa siku au mkeo mwambie mwambie yule mwanamke akae vizuri. HATAKI MTOE. Ndiyo kuikimbia zinaa. Mwili ulivyo nakuambia utakuvuta uangalie hapo hapo. Wewe mwulize mfalmae Daudi atakuambia.
Usizoeane mno na mtu aitwaye konda, au dereva wa bodaboda, au muuza mchicha, au muuza nyanya au muuza uji, nk. Ukiona kuna kitu katikati tafuta mwingine kwani muuza uji au mchija ni mmoja au konda ni mmoja, si wapo wengi huyu ukimwacha kwa muda mrefu akikusahau ndiyo unamrudia akuuzie mchicha au akusaidie na hiyo boda boda yake. Hapo nakufundisha hekima ya kawaida kabisa.
Unamkuta kijana ndiyo vivyo hivyo mjinga mjinga, tu. Ngoja nikupe mfano huu uone mfano wa kijana huyu Biblia inasema hana akili, yaani moko hivi.
“Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake. Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili, Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani.Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo; Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya, Kwangu ziko sadaka za amani; Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu; Ndiyo maana nikatoka nikulaki, Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona. Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari. Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini. Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, Tujifurahishe nafsi zetu kwa mahaba. Maana mume wangu hayumo nyumbani, Amekwenda safari ya mbali; Amechukua mfuko wa fedha mkononi; Atarudi wakati wa mwezi mpevu. Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda. Huyo akafuatana naye mara hiyo, Kama vile ng’ombe aendavyo machinjoni; Au mpumbavu kuadhibiwa katika pingu; Hata mshale umchome maini; Kama ndege aendaye haraka mtegoni; Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.Basi, wanangu, nisikilizeni sasa, Mkayaangalie maneno ya kinywa changu. Moyo wako usizielekee njia zake, Wala usipotee katika mapito yake. Maana amewaangusha wengi waliojeruhi, Naam, jumla ya waliouawa naye ni jeshi kubwa.Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti.” (Mithali 7:4-27).
Umeiona hiyo mistari? Ukiipitia hiyo mistari utaona hiki ninachokufundisha. Dhambi ya zinaa inatakiwa ikimbiwe nakuambia. Huyo ndugu alijikuta kaingia kwenye uzinzi kisa, hakukimbia alipofuatwa tu na huyo mwanamke alikaa akisikiliza, anapigwa busu, yupo tu mwisho wa siku kajikuta kafanya uzinzi.
Naamini umenielewa.
Mungu akubariki
Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

1.Website yetu ya www.mwakatwila.org
2.YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
3.Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga au andika “SOMA NENO LA MUNGU”
4.DVDs📀 au CDs💿
5.VITABU
6.Kwa njia ya Redio:-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.
7.Unaweza kutupata kwenye radio yetu online ya. radio.mwakatwila.org
Kwa mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255754849924 - +255756715222
Wako
Mwl Steven & Beth Mwakatwila.
22/12/2018
No comments:
Post a Comment