Thursday, January 17, 2019

7⃣ MAMBO MUHIMU UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI

Na: MWL STEVEN & BETH MWAKATWILA

FUATANA NASI FACEBOOK

FUATANA NASI YOUTUBE

FUATANA NASI INSTAGRAM

FUATANA NASI ONLINE RADIO
👉🏼 radio.mwakatwila.org

4 Jan, 2019

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana. Ni imani yangu kuwa Mungu amekuvusha salama kuingia mwaka huu mpya wa 2019. Nilibanwa mno na maandalizi pia na kambi ya maombi.

Nikashindwa kukuletea mfululizo wa somo nililokuahidi kukufundisha ili uanze kuishinda dhambi ya uzinzi.

Katika somo lililopita nilikufundisha kuhusu kuikimbia zinaa. Pia kumbuka tunaangalia eneo la chanzo cha uzinzi kinachotokea mwilini.

Nataka nikuonyeshe jambo lingine ambalo unatakiwa ulifanye ili uanze kuishinda hii dhambi.Nalo ni hili.


       JIFUNZE KUISHUGHULIKIA AKILI AU UFAHAMU WAKO.


Angalia maneno haya. “Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa. Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda, na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;ambao wakijua sana hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.” (Warumi 1:18-32).

Ukiisoma hiyo mistari kwa kutulia utaona chanzo kikubwa cha hao watu kujikuta wakiyafanya mambo hayo mabaya ya uzinzi mbaya kabisa yaani kuwa mashoga n.k kilitokana na mfumo mzima wa ufahamu au akili zao zilizokuwa za kijinga au mbovu.

Sikiliza, hao ndugu walimkataa Mungu kwenye eneo la akili zao. Angalia maandiko yanasema hivi. “Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,.......wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye kuvunja maagano,” (Warumi 1:28-32)

Watu hao walikuwa na tatizo kwenye akili zao. Ukiangalia neno akili ndani yake kumebebwa mambo haya:- kuelewa, kujua, ujuzi, ufahamu, and fikra, nia, dhamiri, mawazo na kutambua.

Kuna kitu hapo nataka nikufundishe, unaweza kuokoka lakini ndani ya ufahamu wako usishangae ukawa umemkataa Mungu.

Ukijiuliza swali hili kwanini watu waliokoka wanatenda dhambi ya uzinzi? Jibu mojawapo unaloweza kupewa ni hili WANA MATATIZO KWENYE AKILI AU UFAHAMU WAO. Unaweza kumkubali Mungu lakini akilini mwako ukamkataa kabisa na ukajikuta unazifuata akili zako zisizofaa.

Ngoja nikuonyeshe kitu hiki, Biblia inapozungumzia uzinzi inaonyesha wazi kuwa mtu aufanyao huo uzinzi tatizo lake lipo kwenye akili zake. Angalia hii mistari. “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.(Mithali 6:32)

Angalia na mistari hii. “Maana katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake;Nikaona katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na akili,Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu, Akamwambia kwa uso usio na haya,” (Mithali 7:8-13).

Nimekuonyesha mistari hiyo michache kati ya mistari mingi inayozungmzia habari za mzinzi na mfumo wa akili zake zilivyo.

Neno la Mungu linazungumzia wazi kuwa kitendo cha mtu kuwa mzinzi linatokana na mfumo wa akili zake zilivyo. Biblia inamwita huyo mtu mjinga au asiyekuwa na akili.

Ngoja nikuonyeshe mfano huu utanielewa. Fikiria kidogo mwanaume anamwakia tamaa mwanaume mwenziwe na anamuoa eti ni mke wake. Huyo mwanaume kabeba maua na watu wanamwimbia anameremeta anaolewa na mwanaume mwenziwe unafikiri huyo mwanaume anaeoa na anayeolewa tatizo lao liko wapi?

Tatizo lao liko kwenye akili au ufahamu wao. Mungu anasema ASIYEKUWA NA AKILI au UFAHAMU. Anasema walizifuata akili zao ZISIZOFAA.

Ninapokuambia anza kushughulikia akili zao sijakosea ni kweli. Ukiokoka na bahati mbaya akili zako zikawa na shida fahamu utajikuta unazini na ukafanya uasherati wa ajabu mno.

Ufahamu wako ukikaa vizuri utajua au utaelewa kuwa wewe ni mwanaume unahitaji mwanamke, utajua na utaelewa kuwa sehemu isiyo ya asili ya mwanamke matumizi yake ni nini na sehemu ya asili matumizi yake ni nini. Hata kwa mwanamke ni vivyo hivyo.

Ukiwa na tatizo katika ufahamu wako au akili zako fahamu utajikuta unazini. Ukiwa na akili utafahamu au utajua tu kuwa tendo la kuzini ni tendo lisilokubalika. Sasa utalifanya jambo lisilokubalika?

Mwili wa mwanadamu wenyewe unataka kuzini tu, Sasa ikiwa roho ya huyo mwanadamu ina akili au ufahamu haiwezi kuufuata mwili. Ukiona roho (mtu) ya huyo mwanadamu imefanya huo uzinzi fahamu tatizo lake lipo kwenye akili zake.

Ngoja nikupe mfano huu. Angalia mistari hii. “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;” (2 Wakorintho 10:3-5).

Ukiipitia hiyo mistari utagundua kuwa fikra au akili za watu zinaweza kuwa na matatizo kabisaa mpaka zishughulikiwe ndipo mtu huyo anakuwa huru dhidi ya mwili.

Unapookoka fahamu akili zako au mawazo yako au ufahamu wako zinamwitaji Mungu mno ili azihudumie na kuziweka sawa. Sasa watu wengi wameokoka lakini hawana muda wa kumruhusu Mungu ashughulikie akili zao. Ukiitazama hiyo mistari hapo juu unaona moja ya huduma tunayotakiwa tuifanye ni kushughulikia kuanzia mawazo na fikra zetu.

Kwa nini tushughulikie? Ni kwa sababu zinaweza kuwa mateka, na zikiwa mateka fahamu huyu mtu aliyeokoka kabisaa atajikuta ni mtumwa wa dhambi au mtumwa wa mwili.
Angalia mfano huu. Mtume Petro siku moja alijikuta kwenye mawazo yake ambayo ndiyo chanzo cha akili kabanwa na akaanza kulitumikia shauri la shetani kabisa.

Angalia mistari hii. “Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” (Mathayo 16:22-23).

Mawazo  au akili za Petro ndizo zilikuwa tatizo. Bwana alimwambia kuwa tatizo lako Petro huyawazi, yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu. Angalia ufahamu wa Petro ulipokaa vibaya shetani akaingilia kati kumwongoza Petro na akataka kwenda mbele ya Bwana Yesu Kristo.

Shetani leo hupata nguvu ya kuwaongoza watu walio na Bwana Yesu Kristo kabisa kwenye ubaya kwa sababu ya tatizo la akili au mawazo yao kutokukaa vizuri  tu. Ili umrudishe nyuma yako lazima kwanza uanze kushughulikia ngome za mawazoni kwako., kuna vitu vilivyoinuka huko ndani ya fahamu zako na vingine vinataka kuinuka ambavyo vinapelekea fikra zako kutekwa na kuanza kuburuzwa na mwili.

Usiombe fikra au akili zibanwe, utajikuta unazini na mikono, punyeto au kujisaga, huku mtu akiwa na mawazo au fikra eti ana mwanamke au mwanaume kumbe ni mikono yake migumu kama mishikio ya baskeli. Wewe tulia utaona tatizo hapo lipo kwenye akili tu.

Mtu anamtazama mwanamke kwa kumtamani au mwanaume na anakimbilia bafuni kujichua kapaka sabani nk eti anafanya na yule mwanamke au mwanaume ambaye hayupo.

Au mtu anaangalia picha za ngono na anajikuta akizini na picha za hao aliokuwa anawaangalia huoni kuwa tatizo lake hapo lipo kwenye akili zake ziwazazo vitu ambavyo haviko kabisaa.

Ukijifunza kila mara kuombea akili zako Mungu azitawale na ukubali kweli azitawale ufahamu fahamu zako haziwezi kuwa na upumbavu wa namna hiyo. Utajitambua kuwa wewe ni nani, utautambua mwili wako, utajua au kutambua kuutawala mwili, utajua huyu ni mwanamke ambaye ameletwa na Mungu ni msaidie si KUTUMIA MSAADA ILI KUZINI.

Utajua au kufahamu kuwa ohooo mimi ni msichana nimeumbwa na Mungu mzuri na mwili wangu huu amepewa mwanaume mmoja tu, utajua si kila mwanaume ana uhalali wa kuugusa mwili wako; ni mwanaume mmoja tu.

Utajua au utajitambua uthamani wako aliokupa Mungu wa kuitwa mwanamke. Yaani akili zako zikishughulikiwa utaanza kuona wazi kuwa HAUJAUMBIWA WEWE ROHO UTAWALIWE NA MWILI. Bali mwili utawaliwe na wewe.

Ukijua hivyo tu huwezi kuufuata mwili. Tatizo lako hujui kuwa mwili wako wewe (roho) ndiyo unatakiwa uutawale.

Sijui nikuambieje. Mungu aliumba roho akaipa nafsi ambako huko ndiko akili au mawazo yanakaa, akaipa mwili, ROHO YAKO ILIPEWA HIVYO WEWE NDIYO UNATAKIWA UVITAWALE. Siyo mwili ukutawale.

Ndiyo maana nakuambia ukiona mtu anazini fahamu kuna tatizo kwenye ufahamu wake au akili zake.

Katika somo lijalo nitakufundisha namna ya kushughulikia akili ili zijae vizuri.

Mungu akubariki sana.

Ukihitaji masomo yetu unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-

1.Website yetu ya www.mwakatwila.org

2.YouTube - Mwakatwila au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).

3.Facebook ingia katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata maelezo ya kujiunga au andika “SOMA NENO LA MUNGU”

4. Instagram ingia kwa link pale juu au ingia Instagram na andika Steven Mwakatwila

5.DVDs📀 au CDs💿

6.VITABU

7.Kwa njia ya REDIO :-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili  saa tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu usiku mpaka saa nne usiku.

8.Unaweza kutupata kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org

Kwa mawasiliano zaidi Utatupata kwa namba hizi:- +255754849924 - +255756715222

Wako
Mwl Steven & Beth Mwakatwila.
04/01/2019

No comments:

Post a Comment