7⃣ MAMBO MUHIMU
UNAYOTAKIWA UYAFANYE ILI UPATE KUISHINDA DHAMBI YA UZINZI
Na: MWL STEVEN &
BETH MWAKATWILA
FUATANA NASI FACEBOOK
FUATANA NASI YOUTUBE
FUATANA NASI INSTAGRAM
FUATANA NASI ONLINE
RADIO
👉🏼
radio.mwakatwila.org
4 Jan, 2019
Bwana Yesu Kristo
asifiwe sana. Ni imani yangu kuwa Mungu amekuvusha salama kuingia mwaka huu
mpya wa 2019. Nilibanwa mno na maandalizi pia na kambi ya maombi.
Nikashindwa kukuletea
mfululizo wa somo nililokuahidi kukufundisha ili uanze kuishinda dhambi ya
uzinzi.
Katika somo lililopita
nilikufundisha kuhusu kuikimbia zinaa. Pia kumbuka tunaangalia eneo la chanzo
cha uzinzi kinachotokea mwilini.
Nataka nikuonyeshe jambo
lingine ambalo unatakiwa ulifanye ili uanze kuishinda hii dhambi.Nalo ni hili.
JIFUNZE
KUISHUGHULIKIA AKILI AU UFAHAMU WAKO.
Angalia maneno haya. “Kwa
maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu
wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana
yamekuwa dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo
yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi
zake; yaani, uweza wake wa milele na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa
sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali
walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.Wakijinena
kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na
uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya
wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za
mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.Kwa maana
waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala
ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina. Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao
za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya
asili; wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili,
wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo
ya upotevu wao yaliyo haki yao.Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu
zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu na tamaa na ubaya; wamejawa na husuda,
na uuaji, na fitina, na hadaa; watu wa nia mbaya, wenye kusengenya,wenye
kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye
majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio na ufahamu, wenye
kuvunja maagano, wasiopenda jamaa zao, wasio na rehema;ambao wakijua sana
hukumu ya haki ya Mungu, ya kwamba wayatendao hayo wamestahili mauti, wanatenda
hayo, wala si hivyo tu, bali wanakubaliana nao wayatendao.” (Warumi
1:18-32).
Ukiisoma hiyo mistari
kwa kutulia utaona chanzo kikubwa cha hao watu kujikuta wakiyafanya mambo hayo
mabaya ya uzinzi mbaya kabisa yaani kuwa mashoga n.k kilitokana na mfumo mzima
wa ufahamu au akili zao zilizokuwa za kijinga au mbovu.
Sikiliza, hao ndugu
walimkataa Mungu kwenye eneo la akili zao. Angalia maandiko yanasema hivi. “Na
kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate
akili zao zisizofaa,.......wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao, wasio
na ufahamu, wenye kuvunja maagano,” (Warumi 1:28-32)
Watu hao walikuwa na
tatizo kwenye akili zao. Ukiangalia neno akili ndani yake kumebebwa mambo
haya:- kuelewa, kujua, ujuzi, ufahamu, and fikra, nia, dhamiri, mawazo na
kutambua.
Kuna kitu hapo nataka nikufundishe, unaweza
kuokoka lakini ndani ya ufahamu wako usishangae ukawa umemkataa Mungu.
Ukijiuliza swali hili
kwanini watu waliokoka wanatenda dhambi ya uzinzi? Jibu mojawapo unaloweza
kupewa ni hili WANA MATATIZO KWENYE AKILI AU UFAHAMU WAO. Unaweza kumkubali
Mungu lakini akilini mwako ukamkataa kabisa na ukajikuta unazifuata akili zako
zisizofaa.
Ngoja nikuonyeshe kitu
hiki, Biblia inapozungumzia uzinzi inaonyesha wazi kuwa mtu aufanyao huo uzinzi
tatizo lake lipo kwenye akili zake. Angalia hii mistari. “Mtu aziniye na
mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.” (Mithali
6:32)
Angalia na mistari hii. “Maana
katika dirisha la nyumba yangu Nalichungulia katika shubaka yake;Nikaona
katikati ya wajinga, Nikamtambua miongoni mwa vijana, Kijana mmoja asiyekuwa na
akili,Akipita njiani karibu na pembe yake, Akiishika njia iendayo nyumbani
kwake,Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani. Na tazama,
mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;Ana kelele, na
ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake. Mara yu katika njia kuu, mara
viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia. Basi akamshika, akambusu,
Akamwambia kwa uso usio na haya,” (Mithali 7:8-13).
Nimekuonyesha mistari
hiyo michache kati ya mistari mingi inayozungmzia habari za mzinzi na mfumo wa
akili zake zilivyo.
Neno la Mungu
linazungumzia wazi kuwa kitendo cha mtu kuwa mzinzi linatokana na mfumo wa
akili zake zilivyo. Biblia inamwita huyo mtu mjinga au asiyekuwa na akili.
Ngoja nikuonyeshe mfano
huu utanielewa. Fikiria kidogo mwanaume anamwakia tamaa mwanaume mwenziwe na
anamuoa eti ni mke wake. Huyo mwanaume kabeba maua na watu wanamwimbia
anameremeta anaolewa na mwanaume mwenziwe unafikiri huyo mwanaume anaeoa na
anayeolewa tatizo lao liko wapi?
Tatizo lao liko kwenye
akili au ufahamu wao. Mungu anasema ASIYEKUWA NA AKILI au UFAHAMU. Anasema
walizifuata akili zao ZISIZOFAA.
Ninapokuambia anza
kushughulikia akili zao sijakosea ni kweli. Ukiokoka na bahati mbaya akili zako
zikawa na shida fahamu utajikuta unazini na ukafanya uasherati wa ajabu mno.
Ufahamu wako ukikaa
vizuri utajua au utaelewa kuwa wewe ni mwanaume unahitaji mwanamke, utajua na
utaelewa kuwa sehemu isiyo ya asili ya mwanamke matumizi yake ni nini na sehemu
ya asili matumizi yake ni nini. Hata kwa mwanamke ni vivyo hivyo.
Ukiwa na tatizo katika
ufahamu wako au akili zako fahamu utajikuta unazini. Ukiwa na akili utafahamu
au utajua tu kuwa tendo la kuzini ni tendo lisilokubalika. Sasa utalifanya
jambo lisilokubalika?
Mwili wa mwanadamu
wenyewe unataka kuzini tu, Sasa ikiwa roho ya huyo mwanadamu ina akili au
ufahamu haiwezi kuufuata mwili. Ukiona roho (mtu) ya huyo mwanadamu imefanya
huo uzinzi fahamu tatizo lake lipo kwenye akili zake.
Ngoja nikupe mfano huu.
Angalia mistari hii. “Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita
kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo
katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu
kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira
ipate kumtii Kristo;” (2 Wakorintho 10:3-5).
Ukiipitia hiyo mistari
utagundua kuwa fikra au akili za watu zinaweza kuwa na matatizo kabisaa mpaka
zishughulikiwe ndipo mtu huyo anakuwa huru dhidi ya mwili.
Unapookoka fahamu akili
zako au mawazo yako au ufahamu wako zinamwitaji Mungu mno ili azihudumie na
kuziweka sawa. Sasa watu wengi wameokoka lakini hawana muda wa kumruhusu Mungu
ashughulikie akili zao. Ukiitazama hiyo mistari hapo juu unaona moja ya huduma
tunayotakiwa tuifanye ni kushughulikia kuanzia mawazo na fikra zetu.
Kwa nini tushughulikie?
Ni kwa sababu zinaweza kuwa mateka, na zikiwa mateka fahamu huyu mtu aliyeokoka
kabisaa atajikuta ni mtumwa wa dhambi au mtumwa wa mwili.
Angalia mfano huu. Mtume
Petro siku moja alijikuta kwenye mawazo yake ambayo ndiyo chanzo cha akili
kabanwa na akaanza kulitumikia shauri la shetani kabisa.
Angalia mistari hii. “Petro
akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo
hayatakupata.Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo
kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.” (Mathayo
16:22-23).
Mawazo au akili za
Petro ndizo zilikuwa tatizo. Bwana alimwambia kuwa tatizo lako Petro huyawazi,
yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu. Angalia ufahamu wa Petro ulipokaa vibaya
shetani akaingilia kati kumwongoza Petro na akataka kwenda mbele ya Bwana Yesu
Kristo.
Shetani leo hupata nguvu
ya kuwaongoza watu walio na Bwana Yesu Kristo kabisa kwenye ubaya kwa sababu ya
tatizo la akili au mawazo yao kutokukaa vizuri tu. Ili umrudishe nyuma
yako lazima kwanza uanze kushughulikia ngome za mawazoni kwako., kuna vitu
vilivyoinuka huko ndani ya fahamu zako na vingine vinataka kuinuka ambavyo
vinapelekea fikra zako kutekwa na kuanza kuburuzwa na mwili.
Usiombe fikra au akili
zibanwe, utajikuta unazini na mikono, punyeto au kujisaga, huku mtu akiwa na
mawazo au fikra eti ana mwanamke au mwanaume kumbe ni mikono yake migumu kama
mishikio ya baskeli. Wewe tulia utaona tatizo hapo lipo kwenye akili tu.
Mtu anamtazama mwanamke
kwa kumtamani au mwanaume na anakimbilia bafuni kujichua kapaka sabani nk eti
anafanya na yule mwanamke au mwanaume ambaye hayupo.
Au mtu anaangalia picha
za ngono na anajikuta akizini na picha za hao aliokuwa anawaangalia huoni kuwa
tatizo lake hapo lipo kwenye akili zake ziwazazo vitu ambavyo haviko kabisaa.
Ukijifunza kila mara
kuombea akili zako Mungu azitawale na ukubali kweli azitawale ufahamu fahamu
zako haziwezi kuwa na upumbavu wa namna hiyo. Utajitambua kuwa wewe ni nani,
utautambua mwili wako, utajua au kutambua kuutawala mwili, utajua huyu ni mwanamke
ambaye ameletwa na Mungu ni msaidie si KUTUMIA MSAADA ILI KUZINI.
Utajua au kufahamu kuwa
ohooo mimi ni msichana nimeumbwa na Mungu mzuri na mwili wangu huu amepewa
mwanaume mmoja tu, utajua si kila mwanaume ana uhalali wa kuugusa mwili wako;
ni mwanaume mmoja tu.
Utajua au utajitambua
uthamani wako aliokupa Mungu wa kuitwa mwanamke. Yaani akili zako
zikishughulikiwa utaanza kuona wazi kuwa HAUJAUMBIWA WEWE ROHO UTAWALIWE NA
MWILI. Bali mwili utawaliwe na wewe.
Ukijua hivyo tu huwezi
kuufuata mwili. Tatizo lako hujui kuwa mwili wako wewe (roho) ndiyo unatakiwa
uutawale.
Sijui nikuambieje. Mungu
aliumba roho akaipa nafsi ambako huko ndiko akili au mawazo yanakaa, akaipa
mwili, ROHO YAKO ILIPEWA HIVYO WEWE NDIYO UNATAKIWA UVITAWALE. Siyo mwili
ukutawale.
Ndiyo maana nakuambia
ukiona mtu anazini fahamu kuna tatizo kwenye ufahamu wake au akili zake.
Katika somo lijalo
nitakufundisha namna ya kushughulikia akili ili zijae vizuri.
Mungu akubariki sana.
Ukihitaji masomo yetu
unaweza kuyapata kwa njia hizi zifuatazo:-
1.Website yetu ya www.mwakatwila.org
2.YouTube - Mwakatwila
au HUDUMA YA SOMA NENO LA MUNGU (HUSONEMU).
3.Facebook ingia
katika hiyo tovuti au website yetu utaona alama ya facebook(f) like na utapata
maelezo ya kujiunga au andika “SOMA NENO LA MUNGU”

4. Instagram ingia kwa
link pale juu au ingia Instagram na andika Steven Mwakatwila
5.DVDs📀 au CDs💿
6.VITABU
7.Kwa njia ya REDIO :-
➖Rungwe FM 102.5 Kila siku ya Jumapili saa
tatu mpaka saa nne usiku.
➖Baraka FM 107.7 Kila siku ya Jumanne saa kumi na
mbili jioni mpaka saa moja usiku.
➖Bomba FM 104.1 Kila siku ya Ijumaa saa tatu
usiku mpaka saa nne usiku.
8.Unaweza kutupata
kwenye ONLINE RADIO yetu:- radio.mwakatwila.org
Kwa mawasiliano zaidi
Utatupata kwa namba hizi:- +255754849924 - +255756715222
Wako
Mwl Steven & Beth
Mwakatwila.
04/01/2019

No comments:
Post a Comment